Yohana 18:28
Print
Kisha walinzi wakamchukua Yesu kutoka katika nyumba ya Kayafa kwenda kwenye jumba la mtawala wa Kirumi. Nayo ilikuwa ni mapema asubuhi. Wayahudi waliokuwa pale wasingeweza kuingia ndani ya jumba hilo. Wao hawakutaka kujinajisi wenyewe kwa sababu walitaka kuila karamu ya Pasaka.
Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa wakampeleka kwenye ikulu ya gavana wa Kirumi. Ilikuwa ni alfa jiri. Wayahudi waliokuwa wanamshtaki Yesu hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa wachafu kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika sikukuu ya Pasaka.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) Copyright © 2017 by Bible League International; Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica